Mkoa wa Unguja Kusini

Mkoa wa Unguja Kusini nchini Tanzania.
Ramani ya Unguja Kusini.
Pwani ya Paje wakati wa maji kupwa.

Mkoa wa Unguja Kusini ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 72000 na uko kwenye kisiwa cha Unguja.

Makao makuu yako Koani.

Eneo la mkoa ni km² 854 likiwa na wakazi 195,873 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 (115,588 mwaka 2012) wanaoishi katika wilaya mbili ikiwa Wilaya ya Kati yenye wakazi 132,717 (73,346 mwaka 2012) na Wilaya ya Kusini ina wakazi 63,156 (39,242 mwaka 2012) [1].

Wakazi wa eneo hili la kisiwa cha Unguja, mbali na kujishughulisha na uvuvi kwenye Bahari ya Hindi, ni maarufu pia kwa kilimo cha zao la karafuu, zao linalokifanya Kisiwa cha Zanzibar kujulikana zaidi kama kisiwa cha viungo.

  1. https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne