Mlima Hanang ni jina la mlima mkubwa ulioko katika Mkoa wa Manyara nchini Tanzania. Hanang ni mlima wa volkeno ikiwa volkeno ya kusini zaidi kati ya volkeno za Tanzania kaskazini.
Pia yake huwa na kipenyo cha kilomita 10-12, na kreta kwenye kilele huwa na kipenyo cha kilomita 2.[1]
Una urefu wa mita 3,417 juu ya usawa wa bahari.