Mmisionari (au Mwanamisheni) ni mtu wa dini fulani ambaye anafanya kazi ya kuieneza kwa wasio waumini wa dini hiyo. Kwa kawaida mhusika ni Mkristo, lakini si lazima.
Jina linatokana na neno la Kilatinimissio lenye maana ya utume (kutuma au kutumwa).[1]
↑Barua ya padri Andreas Amrhein kwa Papa Leo XIII tarehe 18 Aprili 1887 kuhusu mazungumzo yake na mkoloniKarl Peters:
"Wao wanataka wamisionari kwa ajili ya faida yao wenyewe. Lakini nimeweka masharti: wamisionari wafanye kazi yao kwa uhuru wote, bila kupingwa kwa namna yoyote na wakoloni. Licha ya hayo naona kwamba wamisionari wataweza kuwalinda wenyeji wasinyonywe ovyo na wakoloni na wafanyabiashara".