Mnazi (Cocos nucifera) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mnazi (Cocos nucifera) ni kati ya miti muhimu zaidi kwa ajili ya uchumi wa kibinadamu katika nchi za tropiki.
Mnazi ni mmea wa familia ya Palmae (au: Arecaceae). Asili yake inafikiriwa iko Asia ya kusini lakini umesambaa tangu karne nyingi sana. Mbegu wake unaweza kuzaa hata baada ya kukaa kwenye maji ya bahari kwa muda fulani hivyo inawezekana ya kwamba mnazi ulisambaa peke yake kwenye pwani za bahari. Lakini bila shaka watu waliibeba safarini kwa sababu ni chakula.