Mnjegere wa kizungu (Pisum sativum) | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Mnjegere wenye makaka
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Mnjegere wa kizungu (Pisum sativum) ni mmea wa mazao wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae unaopandwa mahali popote kwenye maeneo ya tabianchi fufutende. Mbegu zake huitwa njegere za kizungu na huzaliwa katika makaka.
Kuna aina mbili za mnjegere ambazo hukuzwa sana kwa makaka mabichi yao yanayolika. Zote mbili huitwa mnjegere sukari lakini zinatofautiana kwa umbo wa makaka. Pisum sativum var. saccharatum una makaka bapa na P. s. var. macrocarpon una makaka manene.