Mofolojia (kutoka maneno ya Kigiriki morphe, umbo, na logos, neno) au sarufi maumbo ni tawi la isimu ambalo huchunguza maneno ya lugha fulani na aina zake za maneno, hasa upande wa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno.
Mofolojia ni taaluma ya isimu ambayo inachunguza maumbo ya maneno ama maneno kamili yanayobeba maana.
Mambo ya maneno ni matokeo ya muunganiko wa fonimu mbalimbali ambazo pia huungana na kuunda - hatimaye na kuwa neno. Yaani, Fonimu ---> Silabi ---> Neno.