Monie Love | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Simone Gooden |
Pia anajulikana kama | Monie Love |
Amezaliwa | 2 Julai 1970 |
Asili yake | London, England |
Aina ya muziki | Hip hop BritHop New jack swing |
Kazi yake | Rapa, mwimbaji wa hip hop |
Miaka ya kazi | 1989–hadi sasa |
Studio | Warner Bros. Records Cooltempo/Chrysalis/EMI Records Tuff Groove |
Ame/Wameshirikiana na | Native Tongues Dave Angel |
Simone Gooden (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Monie Love; amezaliwa 2 Julai 1970) ni emcee kutoka nchini Uingereza na mtangazaji wa redio wa zamani huko nchini Marekani.
Alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika hip hop ya Kiingereza, na kuleta mgongano/athira kubwa na wasaili/maemcee wengine wa kike wa Kimarekani kama vile Queen Latifah, vilevile kupitia uanchama wake na baadhi ya makundi mwishoni mwa miaka ya 1980/mwanzoni mwa miaka ya 1990 - Native Tongues. Love alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza wa BritHop kuingia mkataba na kusambaziwa kazi zake dunia nzima na mastudio makubwakubwa duniani.