Jiji la Moroni | |
Mahali pa mji wa Moroni katika Komori |
|
Majiranukta: 11°41′35″S 43°15′15″E / 11.69306°S 43.25417°E | |
Nchi | Komori |
---|
Moroni (kwa Mwandiko wa Kiarabu: موروني) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Komori wenye wakazi 60,200.
Mji uko upande wa magharibi wa kisiwa cha Ngazija (Grande Comore). Kuna bandari kwa usafiri kwa meli kwenda visiwa vingine vya Bahari Hindi pia bara la Afrika ya Mashariki pamoja na uwanja wa kimataifa wa ndege.
Anwani ya kijiografia ni 11°45′S 43°12′E.