Mr. Blue | |
---|---|
![]() Mr. Blue kwenye pozi.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Kheri Sameer Rajabu |
Amezaliwa | 14 Aprili 1987 |
Aina ya muziki | R&B na Bongo Flava |
Kazi yake | Mwimbaji |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1999- |
Studio | G. Records, Dhahabu Records, 41 Records |
Ame/Wameshirikiana na | TID Lady Jay Dee, K-Lyin |
Khery Sameer Rajab (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mr. Blue; amezaliwa 14 Aprili 1987) ni msanii wa muziki wa R&B na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania.
Alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa huku akipendwa na wapenzi na mashabiki wa muziki wake, mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake 'Mr Blue'. Ambapo baadaye ikaja kuwa kama ndiyo jina lake la kisanii.
Mr Blue alikuwa gumzo kabla ya kuja kupata umaarufu zaidi na wimbo wake wa 'Mapozi', ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi na sauti aliyotumia pamoja na maujanja ya ala ya muziki wenyewe.