Mshambuliaji

Winga Nani akijaribu kufunga goli kwa kumkwepa beki Philipp Lahm (kulia).
Mshambuliaji (10, jezi nyekundu) kamtoka beki (16, jezi nyeupe) na yupo tayari kupiga shuti kujaribu kufunga. Golikipa naye atajitahidi kuzuioa goli kwa kutokuruhusu mpira usivuke mstari wa goli.

Mshambuliaji (kutoka kitenzi “kushambulia”) ni mchezaji wa nafasi ya mbele anayetakiwa kufunga goli katika michezo mbalimbali kama vile: mpira wa miguu, raga, hoki ya ugani. Hivyo anacheza karibu na goli la timu pinzani akiwa na majukumu makubwa ya kufungia timu yake.

Nafasi yake uwanjani na kazi ndogo ya ukabaji awapo michezoni humaanisha mshambuliaji ndiye wa kufunga magoli mengi zaidi kwa niaba ya timu nzima na wachezaji wenzake.

Mfumo wa kisasa kwa ujumla hutumia mshambuliaji mmoja mpaka watatu; kwa mfano, mfumo uliozoeleka wa 4–2–3–1 hutumia mshambuliaji mmoja.[1][2][3]

  1. Cox, Michael (3 Septemba 2010). "FIFA's 289-page Technical Report on the 2010 World Cup – in 15 points". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-04. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2013.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Cox, Michael (19 Machi 2010). "Is Barcelona's alternative shape really a 4–2–4?". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-02-21. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2013.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Cox, Michael (5 Machi 2010). "Teams of the Decade #5: Roma, 2007". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-26. Iliwekwa mnamo 17 Agosti 2013.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne