![]() | Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Msumenonyororo (kutoka maneno : msu + meno + nyororo; pia msumenomashine na chensoo kutoka Kiingereza "chainsaw") ni pembejeo muhimu sana kwa watu wanaofanya kazi za kukata au kupogoa miti, kukata matofali na pia kuchonga barafu kama inavyofanyika katika nchi Ufini wakati wa majira ya baridi. Msumenonyororo pia hutumika katika nchi baridi kuogelea, hasa wakati wa majira ya kipupwe. Msumenonyororo huwa kifaa kinachoweza kubebwa kwa urahisi, chenye meno makali yanayoweza kuzunguka huku yakikata na kusaga mbao kuzifanya ziwe ndogo.