Mto Ruhwa

Mto Ruhwa (pia: Lua, Luha, Luhwa, Luwa na Ruwa) unapatikana nchini Rwanda na Burundi.

Ni tawimto la mto Ruzizi ambao hutiririsha maji yake hadi kuingia katika ziwa Tanganyika. Kutoka huko maji yanaelekea mto Kongo na hatimaye Bahari ya Atlantiki.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne