Mto Njombe

Mto Njombe ni mto wa Tanzania unaoanzia katika mkoa wa Mbeya, unapitia mpakani mwa mkoa wa Singida na mkoa wa Iringa. Hatimaye huingia katika mto Kisigo, tawimto la Ruaha Mkuu, unaotiririka hadi kuingia mto Rufiji ambao unaishia katika Bahari Hindi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne