Mto Omo unapatikana nchini Ethiopia na unamwaga maji yake katika ziwa Turkana: ndio mto unaochangia kwa wingi zaidi (90% hivi) ziwa hilo lililo kubwa kuliko maziwa yote ya jangwani duniani kote.
Pia ndio mto mkubwa zaidi (km 760) kati ya ile ya Ethiopia nje ya beseni la Naili[1].
Matawimto yake ni Mto Usno, Mto Mago, Mto Neri, Mto Mui, Mto Mantsa, Mto Zigina, Mto Denchya, Mto Gojeb, Mto Gibe, Mto Gilgel Gibe, mto Amara, mto Alanga, Mto Maze na Mto Wabe.
Upande wa chini wa bonde lake umeorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.