|
Mumias Sugar FC ilikuwa klabu ya kandanda nchini Kenya iliyoanzishwa mwaka wa 1977 na makao ilikuwa mjini Mumias. Uwanja wake wa nyumbani ulikuwa Mumias Sports Complex. Ilikuwa mwanachama wa zamu wa divisheni ya juu zaidi katika kandanda ya Kenya, lakini klabu hii ilivujwa katikati mwa msimu wa 2007
Klabu hii ilishinda Kombe la Rais miaka ya 1996 na 1999, ingawa ushindi wa pili ulitupiliwa mbali kutokana na kashfa ya udanganyifu wa mechi
Klabu hii ilikuwa inamilikiwa na Mumias Sugar Company.