Muziki wa Kigregori ni aina nyofu ya muziki wa Kikristo inayotumia sauti moja tu tena bila ya kusindikizwa na ala yoyote.
Ndio muziki rasmi wa Kanisa la Kilatini[1] ambao ulistawi Ulaya magharibi na ya kati katika karne ya 9 na ya 10.
Jina linatokana na hadithi ya kwamba Papa Gregori I ndiye aliyeagiza utumike kanisani.