Mwalugulu ni kata ya Wilaya ya Msalala katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 22,785 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,054 waishio humo.[2]
Mwaka 1982 walinzi wa Sungusungu waliundwa katika mkutano uliofanyika kwenye eneo la kata hiyo.[3]