Mwanasayansi ni mtu anayejihusisha na shughuli maalumu ili kupata maarifa. Kwa maana pana zaidi, mwanasayansi anaweza kutajwa kama mtu anayetumia mbinu za kisayansi.[1] Mtu huyo anaweza kuwa mtaalamu katika eneo moja au zaidi ya sayansi.[2]
Wanasayansi hufanya utafiti kuelekea uelewa mkubwa zaidi wa uasilia, ikiwa ni pamoja na ulimwengu kimwili, kihisabati na kijamii. Kwa kawaida wanasukumwa na udadisi wao.