National Alliance Party of Kenya

National Alliance Party of Kenya (NAK) ilikuwa maungano ya vyama vya kisiasa nchini Kenya yaliyoanzishwa kabla ya uchaguzi wa rais na bunge wa mwaka 2002. Kusidi lake lilikuwa kuunganisha vikundi vyote vilipinga utawala wa rais Daniel arap Moi na chama chake cha KANU. NAK ilikwisha mwaka uleule katika ushirikiano wa NARC.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne