Nazareti (الناصرة kwa Kiarabu, נצרת kwa Kiebrania) ni mji wenye watu 77,445[1] upande wa kaskazini wa nchi ya Israeli, ambao kihistoria unajulikana kama Galilaya.
Wakazi wengi ni raia wa Israeli wanaoongea Kiarabu na kufuata dini za Uislamu (68,7%) na Ukristo (31,3%).
Nazareti unajulikana kama mji walipokulia Bikira Maria na mwanae Yesu Kristo, ambaye kadiri ya Injili, ingawa alizaliwa Bethlehemu, alikuwa anatajwa kama Mnazareti.