Nazari na Chelsi (walifariki labda Milano, Italia, 304 hivi) walikuwa Wakristo waliofia imani yao wakati wa dhuluma ya Dola la Roma.
Ambrosi aligundua masalia yao mwaka 395[1], lakini habari nyingi juu yao hazina msingi katika historia[2][3].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na wengineo kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Julai[4].