Nelson Mandela | |
![]() | |
Rais wa Afrika Kusini (1994-1999)
| |
Deputy | Thabo Mbeki F. W. de Klerk |
---|---|
mtangulizi | F. W. de Klerk |
aliyemfuata | Thabo Mbeki |
tarehe ya kuzaliwa | 18 Julai 1918 Mvezo, Afrika Kusini |
tarehe ya kufa | 5 Desemba 2013 Johannesburg, Afrika Kusini |
chama | African National Congress |
ndoa | Evelyn Ntoko Mase (1944–1958) Winnie Madikizela (1958–1996) Graça Machel (1998–2013) |
watoto | 6 (Makgatho, Makaziwe, Zenani, Zindziswa) |
mhitimu wa | University of Fort Hare University of London University of South Africa University of the Witwatersrand |
Nelson Rolihlahla Mandela (18 Julai 1918 - 5 Desemba 2013) alikuwa mwanasiasa nchini Afrika Kusini, kiongozi wa mapambano dhidi ya siasa ya ubaguzi wa rangi (Apartheid), mfungwa jela kwa miaka 27 halafu rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia katika nchi yake.
Alikuwa mwanasheria na mwanachama, baadaye kiongozi wa chama cha ANC kilichopigania haki za binadamu wote nchini Afrika Kusini.