Kwa aina ya fasihi simulizi tazama makala ya Ngano (hadithi)
Ngano (Triticum L.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Ngano ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu au punje za ngano ni nafaka ambayo ni chakula muhimu katika sehemu nyingi za dunia hasa kwenye kanda zisizo na joto au baridi kali.
Ngano ni kati ya nafaka muhimu zaidi zinazoliwa na watu pamoja na mhindi na mpunga. Ngano hutumiwa hasa kwa kuisaga kuwa unga. Unga wa ngano hutumiwa kwa mkate, chapati na pasta.