Ngome Kongwe (kwa Kiingereza: Old Fort; pia inajulikana kama Arab Fort, kwa Kiswahili: Ngome ya Kiarabu na kwa majina mengine) ni boma lililoko katika Mji Mkongwe, mji mkuu wa Zanzibar. Ni jengo la zamani zaidi[1] na kivutio kikuu cha wageni wa Mji Mkongwe. Iko mbele ya bahari kuu, karibu na jengo lingine la kihistoria la jiji, Jumba la Maajabu (Ikulu ya zamani ya Sultani wa Zanzibar), na inatazamana na Forodhani Gardens.