Mto Niger | |
---|---|
| |
Chanzo | Futa Djalon, Guinea |
Mdomo | Atlantiki |
Nchi za beseni ya mto | Guinea, Mali, Niger, Benin na Nigeria |
Urefu | 4,374 km |
Kimo cha chanzo | 800 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 6,000 m³/s |
Eneo la beseni (km²) | 1,900,000 km² |
Niger ni mto mkubwa kabisa wa Afrika ya Magharibi na mto mrefu wa tatu barani Afrika ukiwa na mwendo wa km 4.374. Njia yake ni kama upinde ikianza Guinea katika nyanda za juu za Futa Djallon kuelekea kaskazini-mashariki kupitia Mali hadi Niger. Karibu na mji wa Timbuktu inageukia kuelekea mashariki, halafu mashariki-kusini kupitia Benin na Nigeria hadi kufika mdomo wa delta yake kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki.
Kabla ya kufikia Timbuktu (Niger) mto unapanuka kuwa na delta ya barani pia mdomo wake baharini una delta kubwa sana.