Nikolasi wa Myra (pia: Nikola, Nikolaus; kwa Kigiriki: Νικόλαος, Nikolaos; 270 – 6 Desemba 343)[1][2] alikuwa askofu wa mji wa Myra akaendelea kuwa mmoja wa watakatifu maarufu zaidi katika Kanisa kwa maadili yake na kwa maombezi yake mbele ya Mungu[3].
Tarehe 6 Desemba ni sikukuu yake[4] inayosheherekewa na Wakristo Wakatoliki, Waorthodoksi na pia na sehemu ya Waprotestanti katika Ulaya ya kati na kaskazini.