Nomino

Mifano
  • Anna na Juma wanacheza.
  • Gari la Oliver' ni zuri sana.
  • Nyumba yetu ipo mjini.
  • Mbuzi wa jirani yetu.
  • Mti mrefu umekatika.

Nomino (kutoka Kilatini: nōmen, jina) ni aina ya maneno inayotaja jina la mtu, mnyama, kitu, mahali, sifa au wazo. Nomino hutokea kwa umbo la umoja au uwingi: kitu, vitu; mtu, watu.

Nomino pamoja na kitenzi hufanya sentensi, mfano: mtu anatembea.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne