| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Alt for Norge ("Yote kwa Unowe" ni wito wa kifalme) Kiapo kufuatana na katiba ya 1814 : "Enige og tro til Dovre faller" ("Pamoja na waaminifu hadi milima ya Dovre inaporomoka") | |||||
Wimbo wa taifa: Ja, vi elsker dette landet Wimbo wa kifalme: Kongesangen | |||||
Mji mkuu | Oslo | ||||
Mji mkubwa nchini | Oslo | ||||
Lugha rasmi | Kinowe1 (Bokmål na Nynorsk) | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Harald V Jonas Gahr Støre | ||||
Katiba Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
Kutoka maungano na Uswidi 7 Juni 1905 26 Oktoba 1905 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
385,207 km² (ya 673) {{{percent_water}}} | ||||
Idadi ya watu - 2024 kadirio - 2013 sensa - Msongamano wa watu |
5,550,203[1] (ya 116) 5,136,700 14.4/km² (ya 213) | ||||
Fedha | Krone ya Unowe (NOK )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .no2 | ||||
Kodi ya simu | +47
- | ||||
1Lugha rasmi ya Kinowe inapatikana kwa namna mbili: bokmål zaidi kama lugha ya kimaandishi na Nynorsk zaidi kama lugha ya majadiliano ingawa inaandikwa pia. Lugha ya Kisami ni lugha rasmi katika miji 6 na Kifini katika mji mmoja. |
Unowe (auː Norwe, Norwei; kwa Kinorwei Norge/Noreg; jina rasmi ni Ufalme wa Unoweː Kongeriket Norge kwa Bokmål na Kongeriket Noreg kwa Nynorsk) ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini.
Imepakana hasa na Uswidi, ila katika ncha ya kaskazini na Ufini na Urusi pia.
Ina pwani ndefu kwenye Bahari ya Kaskazini na ya Atlantiki.
Visiwa vya Svalbard na Jan Mayen katika bahari ya Aktiki ni maeneo ya Norwei.
Pia visiwa visivyokaliwa na watu vya Bouvet katika Atlantiki ya kusini na Peter I katika Pasifiki ya kusini viko chini ya Unowe.
Nchi inadai pia sehemu ya Queen Maud Land katika bara la Antaktika penye kituo cha kisayansi cha Troll.
Mkuu wake kwa sasa ni Mfalme Harald V.
Bunge huitwa Stortinget na wanachama wake huchaguliwa na wananchi kila baada ya miaka minne.
Sikukuu ya taifa ni tarehe 17 Mei, ambapo husherekewa katiba ya Unowe ya mwaka wa 1814.