Nyoka Mnafiki

Nyoka mnafiki
Nyoka mnafiki wa Taita (Boulengerula taitanus)
Nyoka mnafiki wa Taita (Boulengerula taitanus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Amfibia (Wanyama wanaoanza maisha kwenye maji na kuendelea nchi kavu)
Oda: Gymnophiona (Nyoka wanafiki)
Ngazi za chini

Familia 10:

  • Caeciliidae
  • Chikilidae
  • Dermophiidae
  • Herpelidae
  • Ichthyophiidae
  • Indotyphlidae
  • Rhinatrematidae
  • Scolecomorphidae
  • Siphonopidae
  • Typhlonectidae

Nyoka wanafiki ni wanyama wa oda Gymnophiona katika ngeli Amfibia wafananao na nyoka au nyungunyungu wakubwa. Wanyama hawa si nyoka au nyungunyungu kwa ukweli na hata si Reptilia au Annelida. Wana mnasaba na salamanda na vyura lakini hawana miguu. Mkia wao ni mfupi sana au umetoweka, kwa hivyo kloaka iko karibu na mwisho wa mwili. Hupitisha maisha yao yote wakichimba ardhini lakini spishi za familia Typhlonectidae huishi majini na zina aina ya pezi juu ya sehemu ya nyuma ya mwili ambayo inazisaidia kwenda mbele majini. Macho ya nyoka wanafiki ni wadogo na yamefunika kwa ngozi. Kwa hivyo hawawezi kuona vizuri lakini wanaweza kutambua baina ya nuru na giza. Wanyama hawa wanatokea katika mahali pa majimaji pa tropiki kama Afrika, Asia ya Kusini-Mashariki na Amerika ya Kati na ya Kusini.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne