Orodha hii inataja Mapapa wote wa Kanisa Katoliki. Jina rasmi la cheo hicho kwa Kilatini ni Episcopus Romanus, maana yake Askofu wa Roma.
Inawezekana kuwa Hermannus Contractus alikuwa mwanahistoria wa kwanza kuorodhesha Mapapa bila kuacha pengo. Orodha yake ilikwenda hadi mwaka wa 1049 ikimtaja Papa Leo IX kama Papa wa 154. Kulingana na hesabu hiyo, Papa wa sasa, Fransisko ni papa wa 268.
Hakuna orodha rasmi ya mapapa, ila kitabu cha Annuario Pontificio kinachotolewa na Vatikano kila mwaka kina orodha inayoangaliwa kama rasmi. Kulingana na kitabu hicho, Fransisko ni papa wa 266[1].