Pangani | |
Mahali pa mji wa Pangani katika Tanzania |
|
Majiranukta: 5°24′36″S 38°58′48″E / 5.41000°S 38.98000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Tanga |
Wilaya | Pangani |
Pangani ni mji wa Mkoa wa Tanga, nchini Tanzania, uliopo ufukoni mwa Bahari Hindi kati ya Dar es Salaam na Tanga ukielekea pande zote mbili za mdomo wa mto Pangani.
Leo hii ni mji mdogo mwenye wakazi karibu 8n000 na makao makuu ya Wilaya ya Pangani. Lakini ina historia ndefu, hasa kwa sababu kuna bandari nzuri ya kiasili mdomoni wa mto wa Pangani inayofaa kwa jahazi ndogo.
Majengo mbalimbali ya kale ni ishara ya historia ndefu ya mji huu. Pamoja na Boma, lililojengwa na Waarabu wa Unguja na kutumiwa na wakoloni wa Kijerumani na wa Kiingereza, kuna nyumba za Waswahili.
Eneo la mji limegawiwa kwa kata mbili ambazo ni Pangani Mashariki (pamoja na mji wa kihistoria) na Pangani Magharibi[1].