Papa Fransisko siku alipotangaza watakatifu watangulizi wake Yohane XXIII na Yohane Paulo II (2014). Amevaa kanzu nyeupe kama inavyotumiwa na maaskofu wa Roma tangu karne ya 16.
Kardinali Jorge Bergoglio akiongea na rais wa Argentina, Cristina Fernández de Kirchner.
Papa Fransisko, S.I. (kwa Kilatini Franciscus, jina la awali Jorge Mario Bergoglio) ni askofu wa Roma, na hivyo pia Papa wa Kanisa Katoliki duniani kote, tangu tarehe 13 Machi 2013.
Amemfuata Papa Benedikto XVI akiwa wa 266 katika orodha ya mapapa.