Papa Zosimus alikuwa Papa kuanzia tarehe 18 Machi 417 hadi kifo chake tarehe 26 Desemba 418[1]. Alikuwa na asili ya Ugiriki.
Alimfuata Papa Innocent I akafuatwa na Papa Boniface I.
Alikuwa na tabia kali iliyochangia migongano kati ya Kanisa la Roma na sehemu mbalimbali za Kanisa la Magharibi[2].
Hata hivyo, tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Desemba[3].