Paulino wa Trier (alizaliwa Gascony, Ufaransa[1] - alifariki Frigia, leo nchini Uturuki, 358) alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Ujerumani) kuanzia mwaka 346.
Alitetea imani sahihi dhidi ya Uario, na katika Sinodi ya Arles, iliyoitishwa na kaisari Konstans II ili kumlaani Atanasi wa Aleksandria, alikataa peke yake asijali vitisho wala mabembelezo [2][3].
Kwa ajili hiyo alipelekwa uhamishoni alipofariki baada ya miaka 5 ya mateso[4].
Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini na babu wa Kanisa.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 31 Agosti[5][6].