![]() | |
---|---|
Jina la (IUPAC) | |
RNA, ((2'-deoxy-2'-fluoro)C-Gm-Gm-A-A-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-Am-Gm-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-Gm-Am-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-Gm-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-(2'-deoxy-2'fluoro)U-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-(2'deoxy-2'-fluoro)C-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-Gm-(3'→3')-dT), 5'-ester with α,α'-[4,12-dioxo-6[[[5-(phosphoonoxy)pentyl]amino]carbonyl]-3,13-dioxa-5,11-diaza-1,15-pentadecanediyl]bis[ω-methoxypoly(oxy-1,2-ethanediyl)], sodium salt[1] | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Macugen |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
MedlinePlus | a607057 |
Kategoria ya ujauzito | B(US) |
Hali ya kisheria | ? (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Sindano ya ndani ya vitreous (substansi inayofanana na geli ndani ya jicho) |
Data ya utendakazi | |
Nusu uhai | Siku kumi |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C294H342F13N107Na28O188P28[C2H4O](m+n) (m+n≈900) |
Massi ya molekuli | ~50 kg/mol |
![]() |
Pegaptanib, inayouzwa kwa jina la chapa Macugen, ni dawa iliyotumika kutibu ugonjwa wa kuzorota kwa sehemu ya kati ya retina unaohusiana na umri na unaosababisha unyevunyevu (AMD).[2] Ilitumiwa kwa kudunga sindano kwenye jicho.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutoona vizuri, ukungu kwenye lenzi ya jicho, ambayo inaweza kusababisha upungufu wa kuona (ugonjwa wa mtoto wa jicho), kuvuja damu kwenye utando wa jicho, maumivu ya macho na kuongezeka kwa shinikizo la ndani ya jicho.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha shambulio la mzio mkali (anaphylaxis) na maambukizi ya ndani ya jicho (endophthalmitis).[3] Dawa hii inafanya kazi kwa kuzuia sababu ya ukuaji wa mishipa ya endothelial (VEGF).[3]
Pegaptanib iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka wa 2004.[4] Ingawa iliidhinishwa barani Ulaya mnamo mwaka wa 2006, idhini hii iliondolewa.[5] Nchini Marekani, chupa ya miligramu 0.3 inagharimu takriban dola 780 za Kimarekani. [6] Kufikia mwaka wa 2016, haikuwa ikipatikana tena nchini Marekani.[7]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)