Pere Ermengol

Mchoro wa Vicente Carducho ukionyesha Mt. Petro Ermengol alivyookolewa na Bikira Maria baada ya kunyongwa.

Pere Ermengol, O. de M. (1238 hivi – 27 Aprili 1304) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki kutoka Tarragona, Catalonia, Hispania ambaye alikwenda Algeria na Moroko kukomboa watumwa akanyongwa kwa ajili ya imani yake asife.

Kabla ya hapo aliwahi kuongoza kikosi cha majambazi, lakini baada ya kuongoka alijiunga na Shirika la Bikira Maria wa Mersede na kujitosa katika utekelezaji wa karama yake bila kujali hatari kwa uhai wake[1].

Papa Inosenti XI alimtangaza mwenye heri 28 Machi 1686 halafu mtakatifu tarehe 8 Aprili 1687.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Aprili[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/51075
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne