Petro wa Trevi (Rocca di Botte, Abruzzo, karne ya 11 - Trevi nel Lazio, Italia, 30 Agosti 1052) alikuwa kijana Mkristo aliyeishi kitawa bila makao maalumu baada ya kukataa kuoa[1][2].
Akiwa hajui kusoma wala kuandika, alizingatia upwekeni hekima ya Injili [3].
Alitangazwa mtakatifu na Papa Inosenti III tarehe 1 Oktoba 1215[4][5].
Sikukuu yake ni tarehe 30 Agosti[6].