Polisi

Askari polisi wa Ujerumani.

Polisi (kutoka neno la Kiingereza police lilikopwa kutoka Kifaransa police[1] ambalo awali lilikuwa la Kilatini politia,[2] na kabla yake tena la Kigiriki πολιτεία, politeia, "uraia, usimamizi, ustaarabu wa mjini".[3] Msingi ni neno πόλις, polis, "mji".[4]) ni idara ya serikali ambayo lengo lake ni kutekeleza sheria za nchi,[5] kulinda mali[6] kudumisha usalama na kupunguza vurugu, kutokomeza vifo visivyokuwa vya lazima, pamoja na kuokoa mali.[7][8]

Polisi pekee inaruhusiwa kutumia nguvu katika jamii.

Kwa kawaida polisi hutofautiana na wanajeshi ambao kazi yao ni kulinda nchi dhidi ya wavamizi kutoka nje.

Mara nyingi polisi wanajulikana kuathiriwa na ufisadi kwa kiasi tofautitofauti.

  1. "Police". Oxford English Dictionary. Iliwekwa mnamo 4 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. politia, Charlton T. Lewis, Charles Short, A Latin Dictionary, on Perseus Digital Library
  3. πολιτεία, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
  4. πόλις, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
  5. Walker, Samuel (1977). A Critical History of Police Reform: The Emergence of Professionalism. Lexington, MT: Lexington Books. uk. 143. ISBN 978-0-669-01292-7.
  6. Siegel, Larry J. (2005). Criminolgy. Thomson Wadsworth. ku. 515, 516. Google Books Search
  7. Neocleous, Mark (2004). Fabricating Social Order: A Critical History of Police Power. Pluto Press. ku. 93–94. ISBN 978-0-7453-1489-1.
  8. "The Role and Responsibilities of the Police" (PDF). Policy Studies Institute. uk. xii. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-08-29. Iliwekwa mnamo 2009-12-22. {{cite web}}: External link in |publisher= (help)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne