Ponsyo Pilato

Ecce Homo, mchoro wa Antonio Ciseri unaoonyesha Ponsyo Pilato alivyomtambulisha Yesu kwa watu wa Yerusalemu baada ya kumpiga mijeledi

Ponsyo Pilato (kwa Kilatini Pontius Pilatus; kwa Kigiriki Πόντιος Πιλᾶτος; kwa Kiebrania פונטיוס פילאטוס; alikuwa liwali wa kiroma katika Palestina kwenye miaka 26-36.

Anajulikana kutoka vyanzo mbalimbali, lakini hasa kwa sababu ya Injili kumtaja kama hakimu aliyempeleka Yesu kuuawa msalabani. Vyanzo vingine ni katika maandiko ya Yosefu Flavius, Tacitus na Filo wa Aleksandria.

Waandishi Wayahudi Josephus na Philo wanamwonyesha kama mtawala mkali asiyeheshimu utamaduni na imani ya wenyeji wa Palestina. Baada ya kutumia unyama katika ukandamizaji wa Wasamaria aliitwa kurudi Roma na kufika mbele ya Kaisari. Hakuna habari za uhakika kuhusu maisha yake ya baadaye.

Kanisa la Ethiopia linafuata hadithi ya kwamba aliongoka, hivyo linamheshimu kama mtakatifu.

Kadiri ya mapokeo mengine, alijiua.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne