Preieto na Amarino (walifariki Volvic, 25 Januari 676) walikuwa mmoja askofu wa 25 wa Alvernia, leo Clermont-Ferrand, nchini Ufaransa, na mwingine abati au mlei ambao waliuawa pamoja na matajiri wa mji huo[1][2].
Tangu zamani wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini[3].
Sikukuu yao inaadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Januari[4].