Rasi ya Italia au Rasi ya Apenini ni kati ya rasi kubwa za Ulaya, yenye urefu wa zaidi ya kilomita 1,000 kutoka milima ya Alpi hadi kuishia katikati ya Mediteranea.
Iko kusini mwa Ulaya ikizungukwa na Bahari Mediteranea pande tatu. Umbo lake ni kama mguu unaocheza mpira na mpira ni kisiwa cha Sisilia.
Karibu eneo lake lote ni nchi ya Italia. Maeneo matatu madogo ya kujitegemea ndani yake ni San Marino, Monako na Mji wa Vatikani.
Jina la pili la Rasi ya Apenini linatokana na milima ya Apenini inayovuka sehemu kubwa ya urefu wa rasi. Kaskazini kuna tambarare kubwa lenye rutuba.
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |