Rhine Kaskazini-Westfalia (kwa Kijerumani: Nordrhein-Westfalen, NRW) ni moja kati ya majimbo makubwa ya shirikisho la Ujerumani. Lipo magharibi mwa Ujerumani na idadi ya wakazi ni takriban 18,033,000 waishio katika Jimbo hili: ndilo linaloongoza nchini kwa idadi ya watu.
Mji wake mkuu ni Düsseldorf, lakini mji mkubwa ni Köln (Cologne).