Riadha

Baadhi ya michezo ya Olimpiki.

Riadha ni neno lenye asili ya Kiarabu linalojumlisha aina mbalimbali za michezo za hadhara, kama vile kutembea, kukimbia, kuruka na kurusha kitu. Michezo hiyo yote haihitaji vifaa vingi, hivyo ni rahisi kabisa.

Kihistoria, michezo ya mpango inahesabiwa kuwa imeanza na Olimpiki huko Ugiriki mwaka 776 KK.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne