Richadi wa Andria (Uingereza, karne ya 12 - Andria, Puglia, Italia, 1196 hivi) alikuwa askofu wa Andria kwa zaidi ya miaka 40[1][2].
Alipata umaarufu kwa maadili yake, miujiza mingi, pamoja na juhudi kubwa kwa ajili ya uinjilishaji mpya wa waumini.
Alishiriki mtaguso wa tatu wa Laterano (1179).
Alipokea pia kwa heshima masalia ya wafiadini Erasmo na Ponsyano[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa baada ya kutangazwa rasmi na Papa Bonifasi VIII au Papa Eugeni IV[4].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Juni[5].