Rikardo wa Lucca

Mt. Richard wa Sussex katika dirisha la kioo cha rangi huko St Ricarius Church, Aberford.

Rikardo wa Lucca (Wessex, Uingereza, karne ya 7 - Lucca, Toscana, Italia, 3 Aprili 722) alikuwa Mkristo wa Uingereza ambaye alifuata sana dini yake na hatimaye alifariki wakati wa hija yake kwenda Roma pamoja na wanae wawili wa kiume, Wilibaldi wa Eichstätt na Winibaldi wa Heidenheim.

Kati ya watoto wake, hao na binti mmoja, Walburga wa Heidenheim wanaheshimiwa kama watakatifu, sawa naye mwenyewe[1]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Februari[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/39850
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne