Rock and roll

Elvis Presley ni miongoni mwa wanamuziki maarufu wa Rock n' Roll

Rock and Roll ni aina ya muziki wa rock ulioanza kuundwa kunako miaka ya 1950 na 1960. Muziki wa rock unajumlisha aina nyingi za muziki kama vile muziki wa country, muziki wa folk, muziki wa kwayac, nyimbo za kazi, blues na jazz.

Rock and Roll ulianza kuundwa mwanzoni mwa miaka ya 1950 kutoka katika aina ya muziki uitwao rhythm and blues ambao unaimbwa na waimbaji Weusi wa nchini Marekani. Kwa kipindi hicho, muziki huu ulikuwa mashuhuri kwa Waafrika-Waamerika tu. Baadaye baada kwenye miaka ya 1950 na 1960, Rock and Roll umekuwa mashuhuri nchini Marekani na nchi za Ulaya.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne