Rockstar4000

Rockstar4000
Imeanzishwa 2010
Aina za muziki Bongo Flava
Nchi Tanzania
Mahala Dar es Salaam, Tanzania
Tovuti Tovuti rasmi

Rockstar4000 ni jina la lebo maarufu ya muziki na televisheni kutoka nchini Afrika Kusini na ina tawi dogo nchini Tanzania.

Msanii maarufu ambaye alikuwa na hadi sasa yupo chini ya lebo hii ni Ali Swaleh Kiba ambaye mwaka wa 2017 amekuwa mkurugenzi na mshirika wa kampuni hiyo kwa upande wa Afrika Mashariki. Lebo ipo mjini Johannesburg, Afrika Kusini na mkurugenzi mkuu ni Seven Mosha na Jandre Louw.[1] Kiba na Mosha walikutana wakati wa kampeni za One8 ambayo ilikuwa inasimamiwa na mwanamuziki kutoka Marekani, R. Kelly. Tangu hapo, Kiba akawa chini ya menejimenti ya Mosha kupitia Rockstar hadi 2017 walipomuingiza kama sehemu ya kurugenzi ya Rockstar TV na lebo ya kusimamia wasanii. [2] Msanii Alikiba kwa sasa ameanzisha Record Label yake inayoitwa Kings Music

  1. Kiba kuwa mkurugenzi wa Rocksta
  2. Mfahamu zaidi Christine ‘Seven’ Mosha, meneja wa Alikiba Bongo Five ingizo la February 6, 2017.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne