Rolling Stone ni gazeti la habari za tamaduni mashuhuri kutoka nchini Marekani. Inajishuhulisha sana na makala kuhusu muziki, na vilevile michezo, filamu, na watu maarufu. Pia inajishughulisha na filamu zilizofanya vizuri na ripoti ya mapokeo za muziki, yaani inatoa orodha ya "wasanii wakali/albamu kali za karne", na maoni na majadiliano ya kisiasa.