Romano wa Roma

Sanamu yake.

Romano wa Roma (alifariki Roma, Italia, 9 Agosti 258) alikuwa askari, labda kutoka Corsica (leo nchini Ufaransa) aliyeongokea Ukristo akishuhudia kifodini cha shemasi Laurenti alipouawa kwa kubanikwa kutokana na imani yake katika Yesu.

Romano alipoungama imani hiyohiyo alikatwa kichwa[1].

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu mfiadini, hasa siku ya kifodini chake[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/65600
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne