Roy Abernethy

Roy Abernethy (Pennsylvania, 29 Septemba 1906Jupiter, Florida, 28 Februari 1977, ) alikuwa mtendaji katika sekta ya magari ya Marekani, akihudumu kama Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa American Motors Corporation (AMC) kutoka Februari 1962 hadi Januari 1967. Kabla ya kazi yake katika AMC, Abernethy alifanya kazi na Packard Motors na Willys-Overland. Abernethy alichukua nafasi ya George W. Romney, ambaye alijiuzulu kutoka AMC ili kuwa Gavana wa Michigan.[1]

  1. "Roy Abernethy, 70, Former American Motors Chief". The New York Times. 1 Machi 1977. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne